DKT.MWIGULU NCHEMBA ATEULIWA KUWA WAZIRI MKUU WA TANZANIA.

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

‎Taarifa hiyo imesomwa leo Bungeni jijini Dodoma na Mpambe na Mshauri wa Masuala ya Kijeshi wa Rais, Brigedia Jenerali Nyamburi Mashauri, ambaye aliwasilisha hati maalum yenye jina la aliyependekezwa. Bahasha hiyo maalum ilifunguliwa na Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu, ambaye alilitaja rasmi jina la Dkt. Nchemba mbele ya wabunge.

‎Spika Zungu alieleza kuwa Rais Samia amependekeza Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, kushika wadhifa huo wa juu wa Serikali.

‎Dkt. Nchemba, ambaye amehudumu kama Waziri wa Fedha katika serikali iliyopita, sasa anasubiri kupigiwa kura na wabunge kupitia Azimio la Bunge ili kuthibitishwa rasmi kuwa Waziri Mkuu.

‎Iwapo Bunge litapitisha pendekezo hilo, Dkt. Mwigulu Nchemba atamrithi Mhe. Kassim Majaliwa, ambaye amemaliza kipindi cha miaka 10 katika nafasi hiyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TCCIA YAITAKA SERIKALI KUWEKA MIFUMO YA KISHERIA INAYOLINDA MASLAI YA WAZAWA.