TUTAONGEZA MTAALA WA ELIMU YA UFUNDI NA VITENDO KWENYE SHULE ZA MSINGI, SEKONDARY NA 

Na Mwandishi wetu 

Mgombea wa kiti cha Urais na Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labor Party (TLP) Yustas Rwamugira ameinadi sera ya Chama ya kuongeza Elimu ya ufundi(practical) kwa shule za msingi, secondary na vyuoni lengo ili kuongeza uelewa katika kujitegemea.

Akihutubia katika kampeni za Chama hicho zilizofanyika kwenye viwanja vya Kivule,Jijini Dar es salaam Mgombea huyo Elimu ya watoto na vijana misingi yake ni kwenye ujuzi wa kusoma tu,hivyo wataanzisha utaratibu kwenye shule zote wawe na utaratibu wa kufundisha kwa ujuzi na vitendo.

‎"Tunaporudi kwenye Elimu kijana anajifunza elimu ya darasani tu wakati mwingine hata maabara haipo ya Chama chetu tunasema tutaanzisha hizi shule za msingi,sekondary na chuo wawe na utaratibu wa kuwa shule za ufundi na Elimu ya darasani ili mwanafunzi akimaliza shule awe ameelewa elimu ya kilimo,Ujenzi wa majumba au barabara,mekaniki na kadhalika kwa sababu ameshakuwa na elimu hiyo tangu akiwa mdogo",amesema 

‎‎Rwemagira akaongeza kuwa hakubaliani na malipo ya kulipia Marehemu hospitalini jambo linalowafanya wananchi maskini kuzira au kususia maiti za ndugu na jamaa zao matokeo yake wanazikwa na Jiji.

‎"Tumeshudia watu wakizira Maiti kwa sababu ya gharama,mtu akifariki achukuliwe na kuzikwa bure,jambo hili halitakiwi kutokea".

‎Pia kiongozi huyo ametoa kauli juu ya mikopo yenye riba kubwa yaani kausha damu ambayo imekuwa vilio kwa wanawake na familia za kitanzania.

‎"Shauku yetu ni wananchi wapate mikopo isiyoumiza yenye riba ndogo ndogo,wamama wana vilio na familia zina changamoto kwa sababu ya mikopo ya kausha damu".

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa wanawake na Mgombea wa Jimbo la Ilala Nuru Athumani Mwangira Amesema kuwa Watanzania wanaimbishwa nyimbo ya kuwa nchi yao maskini jambo ambalo sio kweli.

‎"Tunaimbishwa nyimbo za umaskini Mimi nakataa Tanzania sio maskini,naamini Tanzania ina Rasilimali nyingi sana na kila mwananchi anastahili kufaidika nazo".Nuru amesema 

‎Bi Nuru akinukuu maneno ya Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli 

‎"Kuna kiongozi alikuja akakubali maneno ya wapinzani kwamba hii nchi sio maskini akasema hii nchi ni tajiri sana na kila mtanzania mmoja ana uwezo wa kununuliwa gari aina ya NOAH nadhani mnamjua ni Marehemu John Pombe Magufuli kwa amali yake sasa inashindikana vipi kila mtanzania mmoja katika watanzania Millioni 70 akapewa Millioni moja ili iweze kumsaidia katika biashara zake",Ametoa nukuu Bi Nuru.


Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kivule Janeth amewataka wananchi kumpeleka Bungeni tarehe 29,octoba 2025 atahakikisha anaisimamia serikali kujenga barabara na miundombinu bora katika eneo hilo.

‎"Nitaisimamia Serikali katika kuhakikisha barabara zetu zinaimarika ,Nafikiri mnajionea changamoto za miundombinu tunayokabiliana nayo ni mashimo na vumbi ikiwa masika njia hazipitiki tunahitaji kuisimamisha vizuri jabani safari hii tubadilike Wana kivule mnichague Mimi", Janeth alisema

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TCCIA YAITAKA SERIKALI KUWEKA MIFUMO YA KISHERIA INAYOLINDA MASLAI YA WAZAWA.