TCCIA YAITAKA SERIKALI KUWEKA MIFUMO YA KISHERIA INAYOLINDA MASLAI YA WAZAWA.

 Na Ngonise Kahise,Dar es salaam 



Chemba ya biashara,viwanda na kilimo Tanzania(TCCIA) imetoa wito kwa Serikali juu ya kuwepo kwa sheria na sera zitakazotoa kipaumbele kwa wazawa zaidi ili kuhakikisha ushiriki wa Watanzania katika miradi mikubwa ya kiuchumi umekuwa wa dhati na wenye tija zaidi.

‎Akizungumza leo Septemba 23,2025 katika mkutano na Waandishi wa Habari kwenye makao makuu ya Ofisi zao,Gerezani Jijini Dar es salaam Rais wa TCCIA Vincent Minja alieleza wakati sahihi umefika kwa taifa kuwa na sera na sheria mahsus zinazolenga kuwawezesha wananchi kiuchumi.

‎"Tunaipongeza Serikali kwa kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje lakini bado tunakabiliwa na changamoto ya ushiriki mdogo wa Watanzania katika miradi ya kimkakati hivyo ni muhimu sasa kuweka mifumo ya kisheria inayolinda maslai ya wazawa",amesema Minja.

‎Minja amebainisha kuwa sheria zilizopo zina msingi mzuri lakini zinahitaji marekebisho kwa mfano sheria ya Local Content na sheria ya Ununuzi wa Umma(PPRA),Sheria hizo zimeweka msingi wa kulinda wazawa lakini utekelezaji wake unahitaji msukumo mpya ili kuhakikisha Watanzania hawabaki watazamaji katika Uchumi wao.

‎Kiongozi huyo amewataka wananchi kuacha kuwadhalilisha wafanyabiashara wazawa kwenye mitandao ya kijamii na iwapo kuna hoja za msingi watoe malalalamiko yao kwa njia rasmi.

‎“Wafanyabiashara hawa wanatoa ajira, wanachangia mapato ya serikali, na
‎wanahatarisha mitaji yao kwa ajili ya maendeleo ya taifa. Tuwaunge mkono
‎badala ya kuwakatisha tamaa,” amesisitiza Minja.


‎Katika hatua nyingine Rais huyo wa Chemba ya Wafanyabiashara hapa nchini ametumia fursa hiyo kutoa
‎Shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita
‎TCCIA imempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa
‎kuendelea kushirikiana kwa karibu na sekta binafsi, na kuweka mazingira
‎wezeshi kwa biashara na uwekezaji.

“Tunatambua jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuweka mazingira
‎rafiki kwa sekta binafsi, na tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu kwa manufaa”amesisitiza


‎Naye Mwanachama wa TCCIA Maeda Waziri ameiomba Serikali kuharakisha michakato ya malipo kwa wawekezaji wazawa wanaofanya kazi na Serikali.




TCCIA imesisitiza kuwa upendeleo wa wazawa sio dhambi Bali ni mbinu halaliya kiuchumi inayotumika Duniani kote.Sekta  binafsi ni injini ya uchumi na kwa kulindwa,itaendelea kusaidia maendeleo jumuishi ya taifa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii