KAMPUNI YA VIOO NI MOTOO WA KUOTEA MBALI
Na Ngonise Kahise
Kampuni inayofanya kazi ya kutengeneza vioo kwenye majengo mbalimbali inayoitwa Dar es salaam Glass works imetoa wito kwa watanzania,taasisi binafsi na mashirika ya Umma kuwa viwango vya bidhaa zao vina ubora wa Kitaifa na Kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo 2, Septemba 2025 kwenye maonyesho ya Wahandisi,Upanga Jijini Dar es salaam Afisa masoko wa kampuni hiyo Hassanaly Dastoor Talib amesema kuwa usalama ndilo jambo muhimu na wanalolizingatia katika wanapotoa huduma zao kwenye maeneo ya ujenzi.
"Kitu cha kwanza ambacho Dar es salaam glass works tunaangalia kwanza usalama wa jengo,usalama wa watanzania na usalama wa wafanyakazi wetu hivyo waondoe mashaka juu ya utendaji wetu".
 
Aidha amebainisha kuwa kuimarika na uthabiti wa kiwanda na biashara hiyo umeletwa na uzoefu mkubwa walionao juu ya bidhaa hiyo.
"Katika maeneo ya vioo sisi tulikuwa watu wa kwanza kuleta vioo Tanzania yaani kampuni binafsi baada ya serikali kwa hiyo tuna uzoefu zaidi katika sekta ya vioo",alieleza Hassanally.
Pia aliongeza kuwa,"Sisi tunazalisha vioo vyenye daraja la juu sana na vioo viko vya aina nyingi ambavyo tunatumia kutoka na mradi unavyohitaji".
Kampuni hiyo ilianzishwa mwa 1979 hivyo ina uzoefu wa zaidi ya miaka 45 na wamefanya kazi katika miradi mingi ya serikali,biashara na watu binafsi ikiwemo Jengo la Airtel,Ujenzi wa Majengo ya wizara mbalimbali Jijini Dodoma na majengo ya biashara.




Maoni
Chapisha Maoni