MRADI WA OKOA MATUMBAWE WASHIKA KASI NCHINI TANZANIA
Na Ngonise Kahise
Meneja hifadhi Bahari na maeneo tengefu Davis Mpotwa amethibitisha kuwa katika utekelezaji wa Mradi wa kuokoa matumbawe nchini wamefanikiwa kuunganisha jamii,wanasiasa,viongozi mbalimbali wa Serikali na wavuvi ambao wanakutana kwa pamoja na kujadili juu ya uhifadhi wa matumbawe.
Amezungumza hayo leo October 7,2025  kwenye mkutano wa Uhifadhi wa mazalia ya samaki mnazi mmoja Jijini Dar es salaam Mpotwa amesema kuwa  Tanzania imetengeneza mkakati wa Kitaifa wa Uhifadhi wa matumbawe.
Aidha amebainisha kuwa Tanzania tayari ina Kamati ya Kitaifa ya uhifadhi wa matumbawe iitwayo Coral Reef Task force ambayo itasaidia kuunganisha wanasayansi na wavuvi,kutoa taarifa ili Dunia ipate mwenendo mzima wa utunzaji wa mazalia ya samaki(matumbawe)
"Uelewa wa wananchi katika maswala ya matumbawe umeongezeka kwa kiwango kikubwa tofauti na hapo awali ,kwa Tanzania kitu kinachotutofautisha na nchi nyingine tumetengeneza kitu kina itwa Coral reef hubs ambayo lengo lake ni kuunganisha watu mbalimbali na inapatikana katika kila maeneo yanayohusika sana na uvuvi ikiwemo Dar es salaam ,Mtwara,Tanga, Zanzibar na Mafya ambapo imesaidia sana katika utekelezaji wa Mradi huu,"Mpotwa ameeleza.
Vile ville amesema yapo mambo ambayo wamedhamiria kuyafanya ikiwa ni pamoja na kutengeneza mfumo portal, ambao utasaidia wanasayansi wote wanahusika na masuala ya baharini hususani katika masuala ya matumbawe kuwa sehemu ambayo wanahifadhi taarifa zao pamoja na kupakua taarifa kutoka sehemu mbalimbali duniani na kuzitumia kwa ajili yakuhakikisha kwamba jamii inazipata.
"Kikao Cha Leo kinalenga kutoa fursa kwa watanzania kujifunza juu ya uhifadhi wa matumbawe kupitia usomaji wa kimtandao unaweza kujisajili kupitia mtandao kwa kushare link kutoka taasisi mbalimbali za serikali wa wataendae katika vyuo vyao na mashirika yao kuhakikisha kwamba kijana wakitanzania wanapata fursa ya kusoma kozi za online zinazohusu matumbawe jinsi gani yakuhifadhi matumbawe na kutumia taaluma za kisayamsi kuhakikisha matumbawe yanaendwa na kuhifadhiwa," Amesema.
Pia amesema kuhakikisha mazalia ya samaki yanaendelea kuwepo kwa kizazi Cha Sasa na kijacho na kuthamini kile ambacho wamefanya katika miaka hii mitatu iliyopita katika utekelezaji wa mradi kwa pamoja wanaenda kutekeleza mwaka wa nne katika kipindi hiki.
Sanjari na hayo pia amewaasa waandishi wa habari pamoja na jamii nyingine kupata fursa ya kuingia katika mfumo portal kupata taarifa mbalimbali hususan zinazohusu bahari,uchafuzi wa mazingira ili kuwa na takwimu halisi unapotoa kwenye vyombo mbalimbali kama magazeti,tovuti au sehemu mbalimbali kama majukwaa kwa ajili ya jamii.
Ametoa wito kwa jamii kutembelea katika maeneo yanayohifadhi matumbawe. Tanzania ni nchi mojawapo ambayo imehifashi vizuri sana matumbawe yake na kwa kiwango kikubwa hivyo Gf7 wameona ni maeneo ambayo yanafaa kufadhiliwa kuendelea kuhifadhi maeneo haya ambayo kwa muda mrefu yamekua katika hali yake nzuri kama Tanga,Pemba,Unguja,Kilwa,Mtwara na Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine Mtafiti na mwalimu kutoka Chuo Kikuu Cha kilomo Cha sokoine Rose Kicheleri amesema mradi umewasidia kupata taarifa muhimu ambazo zitasidia sana kufanya maamuzi ya uhifadhi wa matumbawe pamoja na kuendeleza matumbawe katika nchini . umekuwa kwa kiasi kikubwa kwan
Ametoa wito kwa jamii kutembelea katika maeneo yanayohifadhi matumbawe,Tanzania ni nchi mojawapo ambayo imehifashi vizuri sana matumbawe yake na kwa kiwango kikubwa hivyo Gf7 wameona ni maeneo ambayo yanafaa kufadhiliwa kuendelea kuhifadhi maeneo haya ambayo kwa muda mrefu yamekua katika hali yake nzuri kama Tanga,Pemba,Unguja,Kilwa,Mtwara na Dar es Salaam.
Naye Mtafiti na mwalimu kutoka Chuo Kikuu Cha kilomo Cha sokoine Rose Kicheleri amesema mradi umewasidia kupata taarifa muhimu ambazo zitasidia sana kufanya maamuzi ya uhifadhi wa matumbawe pamoja na kuendeleza matumbawe katika nchini .
Amesema wamehusika katika tafiti mbalimbali na kupata taarifa ambazo ni nzuri na zote zinasaidia hasa tafiti za matishio na fursa ambazo zinatokana na Matumbawe hasa uelewa wa wadau kutoka ngazi tofauti kuhusu matumbawe, mfano matishio na fursa nyingi sana hizi zinaendana na uchimi wa Buluu kwa Tanzania bara bado hazijaweza kuchukuliwa na wadau mablimbali lakini kwa Zanzibar fursa hizi zinachukuliwa kwa nguvu.
 Hivyo amesema ufanyaji wa maamuzi taarifa hizi zinasaidia katika kutekeleza sera za nchi ili kuweza kuweka nguvu zaidi na nikwa jinsi Gani nchi inaweza kufaidika na haya matumbawe.
"Matishio ni kazi za kibinadamu pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi hizi zinakua katika kazi tofauti kutika ngazi ya chini kabisa kwa wananchi wanatumia matumbawe kupata samaki"
Kwa upande wake Afisa uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya mifugo na uvuvi, Upendo Hamidu amesema kwamba wanaangalia ushiriki wa makundi maalumu hasa wanawake na vijana kwenye kusimamia Matumbawe hasa athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi lakini pia shughuli za tabia nchi zinayaharibu .
Amesema mazalia ya samaki yanasababisha kutupatia kiapato pamoja na ulonzi wabahari lakini chamgamoto zinaathiri wadau mbalimbali waliopo kwenye jamii.
Pamoja na hayo amesema kuwa utafiti tuliofanya kuhusu uelewa wa Matumbawe kwa upande wa wanawake wengi sio waelewa kwasababu wao mara nyinginwanabaki pwani hawaendi kuvua samaki,wakati jaamii wanapokea samaki lakini wao katika Jambo la uharibifu kwa Matimbawe hivyo wanaanda program maalumu zitakazosaidia uelewa wanawake na program ambazo zitakuwa endelevu na yanaendelea kutoa faida zinazotokana na Matumbawe kwa taifa Zima lakini wao wenyewe na jamio kwa ujumla
Maoni
Chapisha Maoni