INEC TOENI TAMKO LA WAZI KWAMBA WANAOKUSANYA VITAMBULISHO VYA WAPIGA KURA WANAVUNJA SHERIA


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof.Ibrahimu Lipumba ametoa wito kwa Tume huru ya Uchaguzi(INEC) kutoa Tamko la wazi kwamba hakuna mtu  anayeruhusiwa kukusanya vitambulisho vya wananchi vya kupigia kura.

‎Amezungumza hayo leo October 4,2025 na wananchi waliojitokeza kwenye kampeni za Chama hicho Mbagala Jijini Dar es salaam Prof.Lipumba amebainisha kuwa INEC inapaswa kusimamia taratibu na sheria bila ubaguzi.

‎"Kuna watu wanavunja taratibu na sheria ,Tume inapaswa kulitamka hili wazi kuna watu wanaenda kukusanya vitambulisho vya kupigia kura,hilo ni uvunjaji wa sheria hivyo Tume itoe tamko la wazi kwamba hakuna anayeruhusiwa kukusanya vitambulisho hivyo na vyombo vya Dola viwakamate wanaofanya kosa hil.Huo ni wito wetu nautoa hadharani lakini pia unafuatiwa na  barua rasmi tunaipeleka Tume ya Uchaguzi,"Prof.Lipumba ameeleza.

‎Proffesa amesema taratibu za Uchaguzi bado zina changamoto lakini  wamejitokeza kushiriki  kwa sababu ya Uzalendo walionao na wana shauku ya kuona nchi inapiga hatua madhubuti za kujenga demokrasia imara.

‎Aidha Lipumba ameongeza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama havipaswi kushiriki shughuli za kisiasa .

‎" kwenye mitandao kulikuwa na kauli za hovyo ambazo zingeweza  kuleta sintofahamu nashukuru msemaji wa Jeshi alitamka kwamba wanajeshi wamekula kiapo kulinda katiba ya nchi wao hawapaswi kujiingiza katika shughuli za kisiasa.Ni muhimu vyombo vyetu vya Dola visishiriki katika shughuli za kisiasa,"amesema Lipumba .

‎Vile vile ameeleza kipaumbele katika ilani ya CUF ni Katiba mpya ambayo watahakikisha imepatikana katiba yenye misingi mizuri ya Demokrasia

‎"Lakini ili tupate katiba inayotokana na maoni ya wananchi ilani yetu ya Uchaguzi inaeleza kwamba Chama cha CUF kikishinda Uchaguzi tutaunda serikali ya umoja wa Kitaifa yenye lengo la kujenga umoja wa taifa letu kwa pamoja tuweze kukamilisha zoezi la kupata katiba yenye misingi imara ya Demokrasia katika nchi yetu", ameeleza.

‎Pia amezungumza kuwa Bandari ni Rasilimali tosha ya kuongeza ajira kwa vijana kwani Tanzania imezungukwa na nchi ambazo hazina bandari .

‎"Tuna bahati nchi yetu ina madini ya kila namna lakini mpaka hivi sasa gesi iliyopatikana kwa wingi katika Bahari ya Hindi mpaka gesi hiyo imeanza kununuliwa miaka ya 2005/2006 leo hii 2025 mpaka hivi leo maamuzi ya kuichimba gesi hiyo na kuweza kuwanufaisha Watanzania namaanisha maamuzi ya mwisho ya uwekezaji mpaka sasa hayajafikiwa",Proffesa amefafanua.

‎Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa Tanzania Ina madini kama Nicol yanayopatikana Kabanga, Graphite yanayopatikana Ruangwa pamoja na Shaba ambapo matumizi ya madini hayo  ni kutengeneza Betri za umeme.

‎"Teknolojia imebadilika magari yanayotengezwa Duniani hivi sasa kwa wingi ni magari ya umeme yanahitaji Betri za umeme Chama cha CUF kinasema  tumejipanga tuweze kutumia Rasilimali hii betri za magari ya umeme ziweze kutengenezwa hapa nchini vijana wetu waweze kupata ajira",amesema Proffesa.



‎Katika hatua nyingine Prof.Lipumba amemnadi Mgombea wa Ubunge Jimbo la Mbagala kupitia Chama hicho Sheikh Said Kinyogoli na kuongeza kuwa October  29 wananchi wajitokeze kwa wingi kumchagua Mgombea huyo anayejua matatizo ya Mbagala.

‎Nae Said Kinyogoli amesema kuwa amekwishakuanza ziara za mtaa kwa Mtaa lengo ni kuwafikia wapiga kura wa Jimbo hilo kirahisi.

‎Kinyogoli amesema ili kuitengeneza Mbagala  wananchi kumpigia kura ili aiboreshe sekta ya Elimu katika Jimbo hilo.

‎"Serikali inatuambia Elimu ni bure,jambo ambalo sio kweli.Hapa tuna shule katika Jimbo letu inaitwa Mikwame Secondary,ile shule walimu ni wachache yaani walioajiriwa na Serikali hawatoshi  kwah hiyo wanachukuliwa Waliimu wa ziada kwa ajili ya kwenda kufundisha hawa walimu wa kukodishwa hawalipwi na Serikali wanafunzi wote wanaosoma Mikwame kila Mwezi wanachangishwa  elfu mbili kwa ajili ya kulipa Waliimu wale halafu tunaambiwa Elimu bure katika nchi hii", Amethibitisha Kinyogoli.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TCCIA YAITAKA SERIKALI KUWEKA MIFUMO YA KISHERIA INAYOLINDA MASLAI YA WAZAWA.