KATAVI YAVUTIA MAMIA YA WATALII WA NDANI KATIKA SIKU YA UTALII DUNIANI.
Na.Happiness Sam- Katavi
Mamia ya watalii wa ndani wamejitokeza leo Septemba 27, 2025 kutembelea Hifadhi ya Taifa Katavi kuadhimisha Siku ya Utalii Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe hiyo kwa lengo la kutafakari na kukumbuka mchango wa sekta ya utalii katika kuchangia kipato cha mtu mmoja mmoja na dunia kwa ujumla.
Akitoa hotuba wakati wa maadhisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko aliwapongeza
TANAPA kwa kufanikisha maandalizi ya siku hiyo katika mkoa huu wenye vivutio mbalimbali vinavyouingizia mkoa mapato na ajira kwa vijana wetu.
“Nitoe wito kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi kushirikiana na TANAPA pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kutunza hifadhi zetu ili ziendelee kuwa kapu la kutuingizia fedha za kigeni”, alisema Mrindoko.
Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara TANAPA, Massana Mwishawa alisema katika kuenzi mchango wa utalii kwenye nyanja mbalimbali za kimais

Maoni
Chapisha Maoni