FAMASIA TABIBU KUCHANGIA UFANISI KATIKA HUDUMA ZA AFYA NCHINI.
Na Ngonise Kahise, Dar es salaam
Wizara ya Afya imeona tija kwa vituo vya Afya binafsi na vya Umma kuanzisha na kutekeleza huduma ya Famasia tabibu ambayo itachangia kuongeza ufanisi katika huduma za afya.
Kauli hiyo imetolewa Leo Septemba 24, 2025 Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Ubungo Mhimbili(MOI)Dkt Mpoki Ulisubisya katika hafla ya Sherehe ya Maadhimisho ya Wafamasia Duniani iliyobeba kauli mbiu isemayao" tukifikiria Afya tufikirie na famasia
" Kauli hii imekuja katika wakati sahihi kuikumbusha Jamii ya Wafamasia juu ya jukumu kubwa lililowekwa juu ya mabega yao kuhakikisha Afya za Watanzania wote zinalindwa wakati wote kwa kuzingatia umuhimu wa Wafamasia katika kutoa huduma kwa Wagonjwa " Amesema Mpoki
Amesema wameona tija kwa Mfamasia kuwa sehemu ya matibabu ya Mgonjwa hivyo Wizara inaendelea kuajiri Wafamasia katika huduma za Afya na kutoa ufadhili wa masomo ya ubobezi na kutambua ubobezi wao ili kuongeza ya Wafamasia wengi zaidi katika Sekta hiyo
Kwa Upande wake Msajili wa Baraza la Famasia Boniface Magige amesisitiza ili wapatikane Sekta inayohudumia Jamii bila kujali Sekta ya Umma au binafsi lazima kupanua wigo wa huduma katika Jamii na kadri wigo wa huduma za kijamii unavyoongezeka ndivyo ajira zinavyoongezeka zaidi.
Hata hivyo ameongeza kuwa katika kuimarisha Afya ya Jamii na Dunia kiujumla eneo la figo ni tatizo kwa Jamii hivyo linahitaji Wafamasia wabobezi katika eneo hilo ili kuhudumia wagonjwa kwa karibu zaidi
" Tunaamini huko tunapoelekea katika masuala ya figo,Moyo na tumbo Wabobezi watakaokuja watafanya kazi nzuri na Jamii itatambua kwa ujumla kazi ya Mfamasia kwani tunajua ukuaji wa taaluma hii unakua kwa kasi"Amesema Msajili
Aidha takwimu za sasa zinaonyesha kuwa Wafamasia wamefikia idadi ya Elfu nne Mia moja ishirini na tatu Nchi mzima na bado wapi wengine wanafanyia wafunzo ya utarajali na wanatarajia kuhitimu hivyo wataongezeka hivyo lazima wajipange kuongeza huduma kwa Jamii
Aidha wito umetolewa kwa Wafamasia kuwa Milango ya fursa imefunguka na katika Maisha ukitaka kufanikiwa Vita unaianzisha mwenyewe halafu wale watakaokuona unapambana watakuongezea nguvu kwa kuwa fursa zinafunguka kadri unavyotoa huduma hivyo Wafamasia wajitokeze kwa wingi kujiendeleza kielimu ndani na nje ya nchi.






Maoni
Chapisha Maoni