MKINICHAGUA HUDUMA ZA AFYA KITONGAA.


Na Ngonise Kahise



Mgombea wa Urais  na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Samia Suluhu Hassan amebainisha kutekeleza mikakati ya kuboresha huduma za afya kwa wazee,wanawake wajawazito,watoto na wenye ulemavu ambapo matibabu yao yatabebwa na mfuko wa huduma za afya.

Akizungumza katika uzinduzi wa Chama cha Mapinduzi leo 28,agosti 2025 kwenye uwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es salaam Dkt.Samia amesema wananchi wakimruhusu kuongoza Tanzania katika awamu nyingine mambo kadhaa atakayoyatelekeza ndani ya siku 100 za kwanza swala la afya litakuwa kipaumbele chake.

"Katika kutekeleza huduma ya afya kwa wote tutazindua rasmi mfumo wa afya kwa wote kwa awamu ya majaribio wazee,watoto,mama wajawazito  na wenye ulemavu watabebwa na Mfuko wa taifa wa bima ya Afya".

Dkt.Samia amethibitisha kuwa deni la taifa ndilo deni dogo likilinganishwa na wastani wa deni hilo kwa upande wa Afrika Mashariki 

"Ndugu wananchi deni la taifa hadi kufikia 2024,kwanza deni la serikali zote duniani ni Asilimia 93 ya pato lote la dunia ukichukua serikali zote za dunia,wakati pato serikali zote za Africa  lilikuwa ni asilimia 67 na kwa upande wa Afrika  Mashariki lilifika Asilimia  67".

 "Tukienda kwa nchi moja moja hapa kwetu nchini Tanzania  lilisalia kuwa asilimia 46 ya pato letu la taifa,hili ndilo deni dogo kuliko yote kwa nchi za Afrika  mashariki",amesema Mgombea huyo.

Katika hatua nyingine Rais  Mstaafu wa  awamu ya nne  Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amesema Dr.Samia amepokea nchi katika mazingira  magumu na amefanikiwa utekelezaji mkubwa wa miradi ya ilani ya uchaguzi  2020 katikati ya wasiwasi na mashaka mengi waliyokuwa nayo baadhi ya watu miaka minne iliyopita".

Aidha Dkt.Kikwete ameitaja miradi kamilifu iliyotekelezwa na Dkt.Samia kuwa ni pamoja na ujenzi wa bwana la kuzalisha umeme la Mwalimu Julias  

"Mama Samia alijikuta Rais ghafla,akiwa ziarani jijini Tanga akaletewa habari kwamba Rais amefariki,akatoa taarifa usiku wa manane lakini alichukuwa muda mrefu kujiimarisha katika nafasi ya Urais,alikuwa kama komando aliyetua kwa mwamvuli wa eneo la mapigano huku akipiga risasi",aliongeza Dkt. Kikwete.















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TCCIA YAITAKA SERIKALI KUWEKA MIFUMO YA KISHERIA INAYOLINDA MASLAI YA WAZAWA.