DKT. BITEKO AELEZA MIAKA 10 YA MAPINDUZI YA MAENDELEO BUKOMBE
Na Mwandishi wetu  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Doto Mashaka Biteko amesema kuwa kwa Serikali ya CCM inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya ya Bukombe ikiwa ni pamoja na kutoa fursa za kukuza uchumi wa Wilaya hiyo. Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 27, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata ya Katente wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu. Amesema mwaka 2015 Kata ya Katente, Igulwa na Kata zote zilizopo maeneo ya mjini zilikuwa na kiwango duni sana cha maendeleo ikilinganishwa na maendeleo yaliyofikiwa sasa.  Amesema  Wilaya ya Bukombe ilikuwa na shule moja ya kidato cha tano na sita, hospitali moja, zahanati nne huku umeme ukiwa katika vijiji saba pekee. Amesema Serikali ya CCM imekuwa ikifanya jitihada kubwa ya  kutekeleza miradi ya maendeleo i...