Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2025

MAJALIWA ASHIRIKI SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS HERMINIE WA JAMHURI YA SHELISHELI

Picha
Na Mwandishi wetu  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na viongozi wa nchi za India, China, Mauritius na Comoro kwenye sherehe za kumuapisha Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Dkt. Patrick Herminie zilizofanyika kwenye Uwanja wa Umoja, jijini Victoria nchini humo. Waziri Mkuu ambaye amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, alikuwa miongoni mwa viongozi hao wakuu wakiwemo Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu na viongozi wa juu kutoka vyama rafiki vya siasa. Rais Herminie aliapishwa jana (Jumapili, Oktoba 26, 2025) kuwa Rais wa sita wa nchi hiyo. Viongozi hao ni Makamu wa Rais wa India, Bw. Chandrapuram Ponnusamy Radhakrishnan; Waziri Mkuu wa Mauritius, Dkt. Navinchandra Ramgoolam; Makamu wa Rais wa Chama cha Chinese People’s Political Consultative Conference (CPPCC) Bw. Gao Yunlong na Rais wa Baraza la Mawaziri la Kamisheni ya Bahari ya Hindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Bw. Mohamed Mbae. Mheshimiwa Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikian...

ELIMU YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAWAFIKIA MAAFISA DAWATI NGAZI YA MIKOA NA HALMASHAURI

Picha
 Na Mwandishi wetu  Wizara ya Nishati imeanza kutoa elimu kuhusu Nishati Safi ya Kupikia kwa Maafisa Dawati wa Nishati Safi ya Kupikia ngazi ya mikoa na halmashauri kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia pamoja na kuwawezesha Maafisa Dawati kutambua majukumu yao katika utekelezaji wa mkakati.. Akifungua mafunzo hayo, wilayani Kibaha mkoani Pwani, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bi. Hadija Mruma ameipongeza Wizara ya Nishati kwa jitihada mbalimbali inazochukua kwa vitendo katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini mojawapo ikiwa ni kuhakikisha elimu na vifaa vya nishati safi ya kupikia vinafika hadi ngazi za Mikoa, Halmashauri na Vijiji. Ameeleza kuwa Mkoa wa Pwani unachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachi wanatumia nishati safi ya kupikia katika ngazi ya taasisi, kaya n.k akitoa mfano kuwa asilimia 76 ya taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 mkoani humo zimeshaham...

SERIKALI ILIVYOBADILI SURA YA AJIRA NA MASLAI YA WATUMISHI WA UMMA.

Picha
Na Mwandishi wetu  KATIKA kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, sekta ya utumishi wa umma imepiga hatua katika kuboresha maslahi, ustawi na mazingira ya kazi ya watumishi wa umma nchini. Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, serikali imeweka msukumo maalum kuhakikisha watumishi wanathaminiwa, wanalindwa na wanapata haki zao kwa wakati. MASLAHI YABORESHWA Waziri Simbachawene anasema Rais Samia amefanya mageuzi makubwa katika eneo la maslahi ya watumishi wa umma. Miongoni mwa hatua hizo ni kupunguza Kodi ya Mshahara (PAYE) kutoka asilimia tisa hadi nane, na kuongeza kiwango cha chini kinachotozwa kodi kutoka Sh. 170,000 hadi Sh. 270,000. Hatua hiyo imewezesha serikali kuwasamehe watumishi kodi yenye thamani ya Sh. bilioni 14.78. Vilevile, Waziri Simbachawene anasema serikali imefuta tozo ya asilimia sita (retention fee) iliyokuwa ikikatwa kwa watumishi walio...

JEMA AFRICA WAZINDUA MFUMO WA ZABUNI WA UNUNUZI WA MAGARI WA MOJA KWA MOJA MTANDAONI ‎

Picha
Na Mwandishi wetu  Kampuni ya Jema Africa imezindua Mfumo wa zabuni wa Ununuzi wa magari moja kwa moja mtandaoni iitwayo Online vehicle Live Bidding System ikiwa ni mara ya kwanza kwa mfumo huu kutumika nchini Tanzania na ukanda wote wa Afrika Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Kampuni ya JEMA AUTO, Bw. Lazaro Lutobeka, alisema mfumo huo ni hatua muhimu katika mageuzi ya kidigitali yanayolenga kurahisisha upatikanaji wa magari moja kwa moja kutoka Japan kwa uwazi, uharaka na gharama nafuu. “Mfumo huu wa mnada wa magari mtandaoni ni wa kwanza wa aina yake nchini. Unamwezesha mnunuzi kushiriki moja kwa moja kwenye mnada halisi wa magari unaofanyika Japan kwa wakati huo huo, bila haja ya kusafiri. Ni mageuzi makubwa yanayolenga kuongeza ufanisi, uwazi na ushindani wa haki kwa wateja wetu,” alisema Bw. Lutobeka. Kwa mujibu wa Bw. Lutobeka, mfumo huu umeunganishwa na zaidi ya minada mikubwa 40 ya magari nchini Japan, na kupitia tovuti y...

WAZIRI WA MAMBO YA NJE AZINDUA MKUTANO WA TCCIA

Picha
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amezindua Mkutano Mkuu Maalum wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) jijini Dar es Salaam, ambapo amesisitiza umuhimu wa taasisi hiyo kuwa injini kuu ya kuimarisha diplomasia ya uchumi nchini.  Mhe. Kombo amesema licha ya mchango wake mkubwa katika kukuza biashara, TCCIA imepoteza fursa muhimu za kimataifa, hivyo ni wakati muafaka kwa taasis hiyo kujipanga upya ili kuwa daraja madhubuti kati ya sekta binafsi na Serikali kwa kuvutia uwekezaji, kutengeneza ushirikiano wa kimataifa, kukuza masoko ya bidhaa nje ya nchi na kuhamasisha matumizi ya teknolojia za kisasa.  Aidha, ameitaka TCCIA kuwa mshauri wa Serikali katika kukuza biashara za kimataifa, kuongoza safari za wafanyabiashara nje ya nchi, na kutoa taarifa sahihi za masoko ya kimataifa. Amesisitiza kuwa Wizara itaendelea kushirikiana kwa karibu na TCCIA kupitia jukwaa la diplomasia ya uchumi ili kuiunganis...

TAASISI ISIYO YA KISERIKALI CIP YATOA TATHMINI YA KURA ZA MAONI YA UCHAGUZI MKUU.

Picha
 Na Mwandishi wetu Takwimu zinaonyesha Asilimia 83 ya Wananchi walioshiriki Kura ya maoni kutoka Mikoa 19 wamethibitisha kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29,2025 kwa kupiga Kura Takwimu hizo zimetolewa na Kituo cha Sera za Kimataifa-Afrika(Centre for International Policy -Afrika CIP-Africa) ambapo kuanzia 30 Septemba hadi Oktoba 5,2025 waliendesha zoezi kura za maoni Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani ili kupata twaswira ya hisia za Wananchi Kuhusu Hali ya kisiasa na mwelekeo wa Uchaguzi wa nafasi za wagombea Kupitia vyama vyao. Akizungumza na Waandishi wa habari leo Oktoba 22,2025 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Tafiti na Uchapishaji wa CIP, Thabit Mlangi amesema wamefanya zoezi la kukusanya Kura za maoni kutoka katika Mikoa 19 Tanzania Bara huku Zanzibari Ikiwa miwili Pemba na Unguja ambapo Jumla ya waliohojiwa ni 1,976, wanawake walikuwa 988 na wanaume 988 Kati ya 1,976 waliohojiwa  "Asilimia 29 walikuwa na umri kati ya miaka 18 hadi...

DKT.NCHIMBI AOMBA KURA DODOMA MJINI, KESHO KUANZA KAMPENI MOROGORO.

Picha
Na Mwandishi wetu  MGOMBEA Mwenza  wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema miongoni mwa mipango ya chama hicho kwa miaka mitano ijayo kikirudi tena madarakani ni kujenga Maktaba ya Taifa mkoani Dodoma. Dkt. Nchimbi ameyasema hayo leo Oktoba 17, 2025, katika mkutano wake wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika Wilaya ya Dodoma Mjini alipokuwa akimuombea kura mgombea urais wa chama chake Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea ubunge na udiwani ikiwa zimesalia siku 12 kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025. “Maktaba hiyo itahifadhi kumbukumbu, nyaraka na maandiko mbalimbali ya kitaifa, na itatumiwa na watafiti, wanafunzi na wananchi kwa ujumla kwa maslahi ya taifa.” Aidha Dkt.Nchimbi ameeleza kuwa Serikali ya  CCM pia imedhamiria kujenga shule mpya za msingi 21 na sekondari 16, madarasa 150, maabara 15 za sayansi na mabweni 17 ili kuboresha mazingira ya elimu na kupunguza msongamano darasani. Hata hivyo baada ya kufanya mkutan...

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025;JAJI OMARI AWAONYA WAANGALIZI WA UCHAGUZI

Picha
  Na Mwandishi wetu   WAANGALIZI wa uchaguzi wa ndani na wa kimataifa wametakiwa kuzingatia sheria za nchi na kuepuka kuingilia au kushiriki katika vitendo vyovyote vinavyoweza kuathiri au kuingilia mchakato wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 wakati wanapotekeleza majukumu yao ya uangalizi. Wito huo umetolewa leo Ijumaa Oktoba 17,2025 na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari, wakati akifungua kikao cha siku moja na Waangalizi hao kwa lengo la kuwapa maelekezo, taarifa muhimu NA itmiongozo kuhusu namna ya kutekeleza majukumu yao ya uangalizi wa uchaguzi kwa mujibu wa sheria. Katika hotuba yake, Jaji Omari amewakumbusha waangalizi hao kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uhuru, na kutokuwa na upendeleo, huku wakizingatia sheria za nchi na Mwongozo wa Waangalizi wa Uchaguzi wa mwaka 2025. “Waangalizi wanapaswa kuepuka kuingilia shughuli za uchaguzi, kutoonyesha dhihaka kwa watendaji wa uchaguzi, au kutoa maelekezo kwa maa...

SERIKALI YAWAFUTA MACHOZI WAFANYAKAZI WA SEKTA BINAFSI KWA KUPANDISHA KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA.

Picha
Na Ngonise Kahise  Serikali ya Awamu ya Sita imefanikiwa kutangaza nyongeza ya Kima cha chini cha Mshahara kwa sekta binafsi ambapo kimepanda kwa asilimia 33.4 hatua inayolenga kuongeza tija na kukuza ari ya wafanyakazi kwa kuongeza tija na uzalishaji. Akitangaza Amri hiyo, leo (17 Oktoba 2025) Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa Habari, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwan Kikwete amesema mchakato wa upangaji wa Kima kipya cha chini cha mshahara umekamilika na kwamba umezingatia mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 39 (1) cha Sheria ya Taasisi za Kazi, Sura 300. “Kwa mujibu wa Amri hiyo, Sekta za Kima cha chini cha Mshahara zimeongezeka kutoka 13 za mwaka 2022 hadi 16 kwa mwaka 2025 na kutoka sekta ndogo 25 za mwaka 2022 hadi 46 kwa mwaka 2025. Aidha, Kima cha chini cha mshahara kimeongezeka kwa wastani wa asilimia 33.4 kutoka Shilingi 275,060/= hadi 358,322/= na kitaanza kutumika rasmi tarehe 1 January, 2026”, am...

MGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA MBAGALA SHEIKH KINYOGOLI ALENGA KUWAKOMBOA WAJASILIAMALI MBAGALA

Picha
  Na Mwandishi wetu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof.Ibrahim Lipumba apita kata kwa kata kumnadi kwa wapiga kura Mgombea wa Ubunge Jimbo la Mbagala Sheikh Said Kinyogoli ‎ ‎Akizungumza na wananchi katika Ziara za kampeni ya kumnadi Mgombea huyo October,12 2025 Mbagala Kiburungwa Jijini Dar es salaam Prof.Lipumba amethibitisha kuwa Sheikh Kinyogoli ni kiongozi hodari mwenye maono makubwa ya kuwatetea wakazi wa Jimbo hilo. ‎ ‎Hata hivyo Mgombea wa Ubunge Jimbo la Mbagala Sheikh Said Kinyogoli ametoa ahadi ya kuanzisha SACCOS ya Jimbo kwa ajili ya wajasiliamali mara baada ya kuapishwa kwenye kinyang'anyiro hicho. ‎ ‎"Wanawake,vijana, bodaboda na wajasiliamali wadogo wadogo wakati wa kulikomboa Jimbo la Mbagala umefika nitaanzisha SACCOS ya Jimbo baada ya kuapishwa na Mbagala tutaitoa mikopo ambayo hakuna yeyote kati yenu atakayepigiwa mnada vitu vyake vya ndani kama ilivyo kausha damu eti kwa sababu ameshindwa kulipa mkopo,ninayoyahaidi yanawezekana na nitakwen...

KUNJE WA AAFP KUANZA KAMPENI KANDA YA ZIWA.

Picha
 Na Mwandishi wetu  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP), Kunje Ngombalemwiru, leo ametangaza kumaliza awamu ya kwanza ya kampeni zake za urais na kutoa tathmini ya mafanikio pamoja na changamoto alizokutana nazo, huku akijiandaa kuanza awamu ya pili ya kampeni kesho katika Kanda ya Ziwa. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Ngombale amesema awamu ya kwanza ya kampeni ilihusisha mikoa kadhaa ikiwemo Ruvuma, Lindi, Kilwa, Makambako na Dar es Salaam, ambapo alikutana na wananchi na kusikiliza kero zao moja kwa moja. Amesema kuwa kwa ujumla kampeni hizo zimepata mafanikio makubwa licha ya changamoto ndogondogo, ikiwemo ajali iliyotokea Makambako, mkoani Ruvuma, ambapo gari la waandishi wa habari lilipata ajali na msanii mmoja kujeruhiwa. Alibainisha kuwa hali ya majeruhi inaendelea vizuri. Katika tathmini yake, Ngombale amesema amebaini mambo mengi yanayowakabili wananchi katika maeneo...

UTAFITI MIAMBA BONDE LA EYASI WEMBERE WATHIBITISHA UWEZEKANO WA UPATIKANAJI MAFUTA

Picha
Na Mwandishi wetu  Utafiti unaofanyika katika  mradi wa kimkakati wa  Eyasi Wembere unaolenga kutafuta mafuta na gesi katika bonde la ufa la Afrika  Mashariki umeonesha matumaini makubwa ya kupatikana kwa Mafuta na Gesi katika bonde hilo. Hayo yamebainika wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa  mradi huo mkoani Arusha wilaya ya Karatu  “Kazi za utafiti wa mradi huu zimeanza mwaka 2015,  tumekuwa tukikusanya data mbalimbali zinazohusiana na uwepo wa mafuta na gesi ambapo baada ya ukusanyaji,  data hizo zilitumika kubainisha miamba tabaka ambayo ina mafuta na tukajiridhisha kwamba katika eneo hili la bonde  ipo miamba ambayo inaweza ikahifadhi mafuta”.Amesema Dkt. Mataragio.  Dkt. Mataragio ameeleza kuwa, data za awali za utafiti zilizoanza 2015 kwa njia ya ndege na uchorongaji visima vifupi ambpo ziligharimu takribani shilingi bilioni nane.  Aliendel...

MRADI WA OKOA MATUMBAWE WASHIKA KASI NCHINI TANZANIA

Picha
Na Ngonise Kahise     Meneja hifadhi Bahari na maeneo tengefu Davis Mpotwa amethibitisha kuwa katika utekelezaji wa Mradi wa kuokoa matumbawe nchini wamefanikiwa kuunganisha jamii,wanasiasa,viongozi mbalimbali wa Serikali na wavuvi ambao wanakutana kwa pamoja na kujadili juu ya uhifadhi wa matumbawe. Amezungumza hayo leo October 7,2025  kwenye mkutano wa Uhifadhi wa mazalia ya samaki mnazi mmoja Jijini Dar es salaam Mpotwa amesema kuwa  Tanzania imetengeneza mkakati wa Kitaifa wa Uhifadhi wa matumbawe. Aidha amebainisha kuwa Tanzania tayari ina Kamati ya Kitaifa ya uhifadhi wa matumbawe iitwayo Coral Reef Task force ambayo itasaidia kuunganisha wanasayansi na wavuvi,kutoa taarifa ili Dunia ipate mwenendo mzima wa utunzaji wa mazalia ya samaki(matumbawe) "Uelewa wa wananchi katika maswala ya matumbawe umeongezeka kwa kiwango kikubwa tofauti na hapo awali ,kwa Tanzania kitu kinachotutofautisha na nchi nyingine tumetengeneza kitu kina itwa Coral reef hubs ambayo lengo l...

RC CHALAMILA AZINDUA PROGRAMU YA KONEKT UMEME, PIKA KWA UMEME

Picha
Na Mwandishi wetu  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Octoba 09,2025 amezindua programu ya Konekt Umeme, Pika kwa Umeme iliyobuniwa na TANESCO katika viwanja vya Mwembe yanga wilaya ya Temeke. Programu ya Konekt Umeme, pika kwa umeme ni gharama nafuu, inaufanisi mkubwa, pia umeme unaotumika ni kidogo sana ukilinganisha na nishati zingine. RC Chalamila amepongeza Wizara ya Nishati, na TANESCO na wadau wote wa maendeleo kwa kuja na wazo hili bunifu lenye lengo la kuongeza upatikanaji wa Nishati safi ya kupikia kwa Watanzania. "Mpango huu ni mwanzo wa zama mpya katika historia ya huduma za umeme nchini unaounga mkono juhudi ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu katika matumizi ya nishati safi". Kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya umeme kupikia unaifanya jamii ya kitanzania kwenda kwenye viwango bora vya maisha. Vilevile RC Chalamila amesema ni ukweli usiopingika umeme ni hitaji muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa nchi lakini maendeleo ya mtu mmoja mmoja. Aidha ...

SHULE ZINAZOTUMIA KUNI KAMA NISHATI YA DHARURA ZAELEKEZWA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

Picha
Na Mwandishi wetu   Mkurugenzi wa Nishati safi ya kupikia, Bw. Nolasco Mlay, ametoa wito kwa shule zote nchini kuhakikisha zinaachana na matumizi ya kuni na badala yake kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia, ikiwemo gesi, majiko banifu, na mkaa mbadala. Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya nishati safi ya kupikia inayotekelezwa chini ya mpango wa CookFund katika Mkoa wa Mwanza, Mlay amesema kuwa shule nyingi bado zinategemea kuni kama nishati ya dharura, hali inayochangia uharibifu wa mazingira na madhara kwa afya ya watumiaji. “Katika ziara hii nimebaini Shule nyingi zinatumia kuni kama nishati ya dharura hivyo nitoe wito kwa uongozi wa shule mkishirikiana na Afisa Elimu kuanza kutumia mkaa mbadala ambao ni rafiki kwa mazingira na unachangia katika kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa." Amesema Mlay Aidha, Bw. Mlay amepongeza baadhi ya shule ambazo tayari zimeanza kutumia nishati safi, ambazo hazifadhiliwi na mradi wa Cookfund ikiwe...

TANESCO KUWAUNGANISHIA WATEJA UMEME NDANI YA SIKU MOJA.

Picha
Na Josephine Maxime, Dar es saaam Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, TANESCO imekuja na program maalumu ya kuwahudumia wateja wao Kwa kuwaunganishia wateja wapya huduma ya umeme ndani ya siku moja, ikiwa ni sehemu ya kusogeza huduma karibu na wateja wao. Akizungumza katika maadhimisho hayo yanayofanyika katika viwanja vya mwembe yanga jijini Dar es salaam Bi. Gowelle ameeleza kuwa TANESCO imekuja na program hiyo ya TANESCO Mtaani kwako kwa lengo la kuwahudumia wananchi wa mkoa wa Dar es salaam ambapo wafanyakazi muhimu wa vitengo mbalimbali vya shirika wameweka kambi kwenye viwaja hivyo kwa siku tatu kuanzia leo Oktoba 08 ili  kutoa huduma kwa wananchi. Vilevile amesema kwa siku ya alhamisi wanatarajia kuwa na hafla ya uzinduzi wa  mpango maalum wa kuwaunganishia umeme wateja wapya na kuwakopesha majiko ya umeme kwa wale watakaopenda kutumia nishati ya umeme kwenye kupika na kwamba watayalipa kidogo kidogo kupitia manunuzi yao ya umeme kwa mkataba wa miezi sita hadi...

MSAJILI HAZINA ASHIRIKI UZINDUZI UJENZI MGODI WA MADINI KINYWE

Picha
Na Mwandishi wa OMH Mahenge, Morogoro. Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ameshiriki uzinduzi wa shughuli za ujenzi wa mgodi wa madini ya kinywe (graphite), uliofanywa na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, katika hafla iliyofanyika Alhamisi, Oktoba 9, 2025, katika eneo la Mahenge, Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro. Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya Faru Graphite Corporation, kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania, kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina (hisa 16%), na Black Rock Mining Limited (hisa 84%), ikiwa ni hatua muhimu katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya sekta ya madini nchini. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Mavunde alisema ujenzi wa mgodi huo unatarajiwa kugharimu takribani $510 milioni (zaidi ya Sh1.3 trilioni). Aliendelea kusema kuwa uwekezaji huo utazalisha ajira zaidi ya 400 wakati wa ujenzi na zaidi ya 900 za kudumu mgodi utakapoanza uzalishaji kamili.  Nje ya mgodi, alisema Mhe. Mavunde, ajira zisizo za moja kwa moja zaidi ya 4,500 zinatar...

WANANCHI ITILIMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUUNDA MFUMO WA MALIPO YA KIFUTA JASHO /MACHOZI

Picha
 WANANCHI ITILIMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUUNDA MFUMO WA MALIPO YA KIFUTA JASHO /MACHOZI Na Mwandishi Wetu- Itilima Wananchi wa vijiji vya Nyantugutu, Lung'wa na Nding'ho vya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu wameipongeza Serikali kwa kuunda na kuboresha   mfumo wa ukusanyaji  wa taarifa  za wanyamapori  wakali na waharibifu (Problem animal information  system- PAIS) ambao umerahisisha malipo ya kifuta jasho/machozi pindi madhara ya wanyamapori wakali na waharibifu yanapotokea kwa wananchi. Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ndi'hgo , Bi. Salome Kambona katika mkutano wa hadhara wa kuelimisha wananchi namna ya kukabiliana na changamoto za wanyamapori wakali na waharibifu uliofanyika kijiji cha Ndi'hgo ,Wilaya ya Itilima leo Oktoba 9, 2025. "Tunaishukuru Serikali kwa mfumo huu ambao ndani ya siku saba mwananchi atatakiwa awe ametoa taarifa ya madhara yaliyotokana na mnyamapori ili aweze kulipwa" amesema Bi.Salome. Naye, Mkazi wa Kijiji cha Ny...