Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2025

MONALISA APINGA VIKALI KUVULIWA ACT

Picha
Na Ngonise Kahise  Kada wa ACT wazalendo Monalisa Ndala  amepinga vikali kuvuliwa kwake uanachama kupitia taarifa zilizotolewa na uongozi wa Chama hicho kwa madai ya kushindwa kutekeleza katiba ya Chama hicho. Akizungumza na waandishi wa habari leo 30,agosti 2025 Sinza,jijini Dar es salaam Monalisa amesema kuwa yeye Bado ni mwanachama wa ACT aliyesajiliwa Dar es salaam na sio Mafifi mkoani Iringa . "Nimempa Katibu Mkuu siku mbili anapaswa atoke hadharani aikanushe ile barua kwa sababu Mimi ni  mwanachama,mwenezi wa mkoa wa Dar es salaam pia ni Mwenyekiti wa Jimbo la kibamba nawezaje kuwa mwananchi wa kata ya Mafifi". "Aibu hii haitasaidia Chama zaidi ya kuishangaza jamii kwa hiyo Katibu Mkuu inabidi anusuru na anapaswa aseme barua sio rasmi na baada ya juma hili nitafuata hatua sahihi  na tusilaumiane".ameeleza Monalisa. Aidha amekitaka Chama kujitafakari na wanachama waone uzembe uliofanywa pia viongozi wanajua kinachofanyika ni hatua za kuimarishana kwani ACT ni C...

MKINICHAGUA HUDUMA ZA AFYA KITONGAA.

Picha
Na Ngonise Kahise Mgombea wa Urais  na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Samia Suluhu Hassan amebainisha kutekeleza mikakati ya kuboresha huduma za afya kwa wazee,wanawake wajawazito,watoto na wenye ulemavu ambapo matibabu yao yatabebwa na mfuko wa huduma za afya. Akizungumza katika uzinduzi wa Chama cha Mapinduzi leo 28,agosti 2025 kwenye uwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es salaam Dkt.Samia amesema wananchi wakimruhusu kuongoza Tanzania katika awamu nyingine mambo kadhaa atakayoyatelekeza ndani ya siku 100 za kwanza swala la afya litakuwa kipaumbele chake. "Katika kutekeleza huduma ya afya kwa wote tutazindua rasmi mfumo wa afya kwa wote kwa awamu ya majaribio wazee,watoto,mama wajawazito  na wenye ulemavu watabebwa na Mfuko wa taifa wa bima ya Afya". Dkt.Samia amethibitisha kuwa deni la taifa ndilo deni dogo likilinganishwa na wastani wa deni hilo kwa upande wa Afrika Mashariki  "Ndugu wananchi deni la taifa hadi kufikia 2024,kwanza deni la serikali zo...

*WAZIRI MKUU ATOA WITO KWA WATUNZA KUMBUKUMBU

Picha
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka  watunza kumbukumbu wote nchini kuzingatia maadili ya kazi, kudumisha uadilifu na kulinda usiri wa taarifa zote zinazohifadhiwa kwani taarifa hizo ni nyenzo muhimu ya usalama wa Taifa na maendeleo ya nchi. Ametoa wito huo leo 27,agosti 2025 katika mkutano mkuu wa 13 wa chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania(TRAMPA) uliofanyika Upanga,jijini Dar es salaam na kusema kuwa chama hicho kina dhamana kubwa ya kuhakikisha nyaraka na kumbukumbu zote muhimu za Serikali pamoja na taasisi binafsi zinatunzwa kitaalamu na zinahifadhiwa kwa weledi wa viwango vya juu. “Utunzaji sahihi wa nyaraka na kumbukumbu ni uti wa mgongo wa uwajibikaji, historia, na utawala bora. Bila masjala madhubuti, Taifa letu lingeweza kukabiliwa na changamoto kubwa za upotevu wa taarifa, ucheleweshaji wa maamuzi, na hatimaye kurudisha nyuma juhudi za maendeleo.” Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa TRAMPA inapaswa kuendelea kuchochea uwajibikaji, utawala bora pa...