MAJALIWA ASHIRIKI SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS HERMINIE WA JAMHURI YA SHELISHELI
Na Mwandishi wetu  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na viongozi wa nchi za India, China, Mauritius na Comoro kwenye sherehe za kumuapisha Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Dkt. Patrick Herminie zilizofanyika kwenye Uwanja wa Umoja, jijini Victoria nchini humo. Waziri Mkuu ambaye amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, alikuwa miongoni mwa viongozi hao wakuu wakiwemo Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu na viongozi wa juu kutoka vyama rafiki vya siasa. Rais Herminie aliapishwa jana (Jumapili, Oktoba 26, 2025) kuwa Rais wa sita wa nchi hiyo. Viongozi hao ni Makamu wa Rais wa India, Bw. Chandrapuram Ponnusamy Radhakrishnan; Waziri Mkuu wa Mauritius, Dkt. Navinchandra Ramgoolam; Makamu wa Rais wa Chama cha Chinese People’s Political Consultative Conference (CPPCC) Bw. Gao Yunlong na Rais wa Baraza la Mawaziri la Kamisheni ya Bahari ya Hindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Bw. Mohamed Mbae. Mheshimiwa Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikian...