DKT ROGERS SHEMWELEKWA AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATA YA PICHA YA NDEGE
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Rogers Shemwelekwa, akiwa ameambatana na Wakuu wa Divisheni na Vitengo mbalimbali, amefanya ziara ya kikazi katika Kata ya Picha ya Ndege yenye lengo lakutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea katika kata hiyo. Katika ziara hiyo, Dkt. Shemwelekwa ametembelea miradi ya uchongaji barabara(milioni 30 mapato ya ndani) ujenzi wa vituo vya kibiashara kwa mbonde ( milioni 562.5 mapato ya ndani) , pamoja na ukamilishaji wa chumba kimoja cha darasa katika Shule ya Msingi Lulanzi ( milioni 8 mapato ya ndani). Aidha, amekagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Wilaya ( Milioni 706.7 mapato ya ndani na Serikali kuu, Ununuzi wa Vifaa tiba,( milioni 300 Serikali kuu) , Ofisi ya Kata ya Picha ya Ndege ( milioni 24.5 mapato ya ndani)na ujenzi wa chumban kimoja Cha darasa shule ya msingi Mkuza (milioni 20 mapato ya ndani) Vilevile, Mkurugenzi huyo alifanya mkutano wa hadhara uliolenga kusikiliza na kutatua kero mbalimbali ...